ZAIDI YA ASILIMIA 60 YA WAGONJWA WA MOYO JKCI WANATOKA KANDA YA KASKAZINI
ZAIDI YA ASILIMIA 60 YA WAGONJWA WA MOYO JKCI WANATOKA KANDA YA KASKAZINI
Na Oscar Assenga, Tanga ZAIDI ya asilimia 60 ya wagonjwa wanaopatiwa huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) wanatoka katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, hali inayoendelea kuchochea ujenzi wa Taasisi kubwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Hospital ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Akizungumza jijini Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Burian wakati wa mkutano wake na wana habari kuelezea harambee ya kuchangia ujenzi wa Taasisi Kubwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Mei 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga Alisema serikali pamoja na wadau wa maendeleo wameona umuhimu wa kuimarisha huduma za moyo Kanda ya Kaskazini kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa kutoka eneo hilo wanaohitaji matibabu ya kibingwa. Alisema mradi huo utakaojengwa KCMC utakuwa na uwezo wa kutoa huduma za kisasa zinazolingana na zile zinazotolewa JKCI, na unatarajiwa kuhudumia wakazi wa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha n…