Posts

WAZIRI NDEJEMBI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BENACO–KYAKA

WAZIRI NDEJEMBI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BENACO–KYAKA
📌 Utawezesha Mkoa wote Kagera kuunganishwa na Gridi ya Taifa 📌 Zaidi ya Bilioni 270 kutumika kutekeleza mradi 📌 Mradi kukamilika ndani ya miezi 24 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Mei 9, 2026 ameweka jiwe la msingi la mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa KV 220 Benaco–Kyaka pamoja na Kituo cha Kupoza Umeme cha Benaco wilayani Ngara, mkoani Kagera. ''Tunatarajia ndani ya miezi 24 Mkoa wa Kagera uwe umeunganishwa katika Gridi ya Taifa na changamoto za umeme ziwe historia,” alisema Mhe. Ndejembi. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Bw. Mathias Kahabi, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nishati kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya umeme wilayani humo. Amesema katika Jimbo la Ngara vijiji vyote 75 tayari vimefikiwa na huduma ya umeme, huku vitongoji 219 kati ya vitongoji 389 vikiwa tayari vimeunganishiwa umeme. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro…