WAZIRI MKUU ASISITIZA USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKABILIANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA, AANGAZIA NAFASI YA TEKNOLOJIA
WAZIRI MKUU ASISITIZA USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKABILIANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA, AANGAZIA NAFASI YA TEKNOLOJIA
▪️︎ Asema mapambano dhidi ya uhalifu yanahitaji mshikamano wa kimataifa ▪️︎ Aeleza teknolojia ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na uhalifu wa kisasa WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ushirikiano wa kikanda na kimataifa ni sharti la mafanikio katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa unaozidi kubadilika na kuvuka mipaka. Amesema kuwa katika dunia ya sasa, aina nyingi za uhalifu hupangwa, hufadhiliwa na kuratibiwa kwa njia za kidijitali, hali inayohitaji mifumo imara ya kiteknolojia pamoja na ushirikiano wa pamoja ili kuudhibiti kwa ufanisi. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Mei 4, 2026, wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 11 na Kongamano la Chama cha Waendesha Mashtaka Afrika Mashariki (EAAP), unaofanyika katika Ukumbi wa Blue Sapphire, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 4 hadi 6 Mei, 2026, wenye kaulimbiu isemayo “Matumizi ya Teknolojia katika Kukabiliana na Uhalifu Dhidi ya Wanyamapori na Uhalifu wa Kimataifa Uliopangwa.” “Kama ambavyo uhalifu uliopangwa hauwezi kuwepo …