WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MCHEPUO YA MJI WA IRINGA
WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MCHEPUO YA MJI WA IRINGA *Asema mradi huo utafungua fursa mpya za uchumi na kupunguza msongamano wa magari mjini Iringa *Aagiza wakandarasi kuwalipa kwa wakati wadaiwa wao WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya miundombinu ili kuboresha usafiri, kuongeza ufanisi wa uchukuzi na kufungua fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi nchini. “Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla. Itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuongeza biashara na kuchochea ukuaji wa mji wa Iringa,” amesema Dkt. Nchemba. Amesema hayo leo Jumamosi, Mei 23, 2026 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mchepuo ya Mji wa Iringa (Iringa Municipal Bypass) yenye urefu wa kilomita 7.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Iringa. Mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya SINOHYDRO Corporation Limited kwa usimamizi wa TANROADS kupitia kitengo chake cha TECU, unagharimu shilingi bilioni 41.6. Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo…