Wauguzi Watatajwa Nguzo ya Uchumi wa Dola Trilioni Moja ifikapo 2050

Wauguzi Watatajwa Nguzo ya Uchumi wa Dola Trilioni Moja ifikapo 2050
UBORA wa rasilima watu( Afya na Maarifa) ndio sarafu ya dunia kwa sasa na hivyo kete muhimu kwa Tanzania kujiunga na Mataifa tajiri mwaka 2050( Trilioni dola Club). Wauguzi ndio Nguzo ya Rasilimali Watu na Mhimili wa Uchumi wa Dola Trilioni 1 (2050) Katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, tunatambua kuwa uuguzi si kazi tu, bali ni wito wa kitume unaohitaji upendo, subira, na utu wa hali ya juu. Wauguzi ni daraja kati ya wagonjwa na kupona, wakiwa mstari wa mbele kuokoa maisha. Bila afya bora, hakuna tija kazini; wauguzi wanahakikisha jamii ina afya, na hivyo kuwa kiungo muhimu kimkakati katika kujenga uchumi mkubwa. Tanzania inalenga kujiunga na "Club" ya nchi zenye uchumi wa kuanzia dola trilioni moja ifikapo 2050. Hata hivyo, ili kufika huko, tunahitaji rasilimali watu yenye afya bora. Pamoja na uwekezaji mkubwa wa kibajeti kuboresha miundomibinu ya huduma, vifaa tiba, dawa, wauguzi na madaktari uliofanywa na Serikali, Bado kuna changamoto kubwa ya uwiano idadi ya wauguz…