WANASIASA WATAKIWA KUHUBIRI AMANI, KIPAUMBELE MAENDELEO
Na.Sophia Kingimali. Mwananchi na mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa, Dk David Msuya, amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia lugha ya staha na busara wanapozungumza na wananchi ili kulinda amani ya Tanzania na kuondoa migawanyiko inayoweza kujitokeza kutokana na matamshi ya kisiasa. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari,leo Mei 22,2026 Dk Msuya amesema licha ya siasa nchini kwenda vizuri kwa ujumla, bado zipo changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi, hususan matumizi ya maneno yenye kuibua taharuki na chuki miongoni mwa wananchi. Amesema baadhi ya kauli kutoka kwa viongozi wa kisiasa zimekuwa zikiumiza mioyo ya Watanzania badala ya kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa. Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, hivyo hakuna sababu ya kutumia siasa kuleta migawanyiko wakati wananchi wanahitaji kuona maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali ikiwemo barabara, afya, elimu na uwekezaji. Alisisitiza kuwa wananchi wanataka kuona miradi ikikamilika kwa wak…