VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPAMBANA NA MATAPELI BIASHARA ZA MITANDAONI
VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPAMBANA NA MATAPELI BIASHARA ZA MITANDAONI
Serikali imewataka Vijana wanaojishughulisha na Biashara za Mitandao nchini kuwa walinzi Wakuu wa mifumo ya kidijitali kwa kupambana vikali na matapeli wa mtandaoni, kwani vitendo vyao vinaharibu uaminifu ambao ndio nguzo kuu ya uchumi wa sasa na wa baadaye. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb) wakati akizungumza katika hafla kubwa ya 'Arise and Shine Recognition Rally 2026' iliyofanyika Mei 24, 2026 katika ukumbi wa The Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa kampuni ya BF Suma. Katika hafla hiyo iliyokusanya zaidi ya vijana 30,000 waliojiunga na mfumo huo, Serikali imebainisha kuwa mustakabali wa ajira na masoko unahama rasmi kuelekea kwenye simu za mkononi, hivyo kulinda uaminifu wa wateja ni suala la kufa na kupona kiuchumi. Londo amewaasa vijana kuvaa 'mabomu' (kujitoa kwa dhati) kupambana na wale wote wanaoharibu imani ya Watanzania kwenye biashara za kidigitali ili kulinda sekta inayotoa maelfu ya ajira. Aidha,…