UPATIKANAJI UMEME KUENDELEA KUIMARIKA MKOANI IRINGA— MHE. SALOME

UPATIKANAJI UMEME KUENDELEA KUIMARIKA MKOANI IRINGA— MHE. SALOME
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Iringa. Amesema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Mkoa wa Iringa umepokea zaidi ya shilingi bilioni 124 kwa ajili ya kuimarisha huduma ya umeme na kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha kujiletea maendeleo ya kiuchumi. Mhe. Salome ameyasema hayo leo Mei 23, 2026 wakati akijibu hoja za wananchi mkoani Iringa, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba. Amesema changamoto za umeme zilizokuwa zikikabili baadhi ya maeneo ikiwemo Kata ya Mafifi tayari zimeshapatiwa ufumbuzi na wananchi wanaendelea kupata huduma ya umeme wa uhakika. Hata hivyo, amesema katika Mtaa wa Mosi huduma hiyo bado haijafika ipasavyo ambapo tayari maelekezo yametolewa kwa TANESCO na REA kuhakikisha wananchi wa eneo h…