TUME YA MADINI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA IDRAS KUONGEZA UFANISI, MAPATO
TUME YA MADINI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA IDRAS KUONGEZA UFANISI, MAPATO
Arusha Tume ya Madini imeanza rasmi kutumia Mfumo Jumuishi wa Kodi za Ndani (IDRAS) unaolenga kurahisisha utoaji wa huduma, kuongeza ufanisi wa utendaji na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika sekta ya madini. Akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha wahasibu na wachumi wa Tume ya Madini kilichomalizika leo mkoani Arusha kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Nsajigwa Kabigi, amesema mfumo huo utawawezesha wateja kujihudumia saa 24 popote walipo na kuharakisha utoaji wa huduma. Amesema matumizi ya IDRAS yataongeza ufanisi katika usimamizi wa mapato huku yakirahisisha huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini. “Tunatarajia mfumo huu kuongeza mapato ya Serikali na kuwapa wateja huduma kwa haraka na urahisi zaidi,” amesema Kabigi. Kabigi pia amewataka wahasibu na wachumi kuwa makini katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa kuzingatia usalama wa taarifa na nyaraka zinazotumika kupitia mfumo h…