Tanzania na Rwanda Zaimarisha Ushirikiano: Biashara, Nishati na Udugu wa Kihistoria Wawekwa Mbele

Tanzania na Rwanda Zaimarisha Ushirikiano: Biashara, Nishati na Udugu wa Kihistoria Wawekwa Mbele
Na Janeth Raphael- MichuziTv Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda hauishii kuwa wa ujirani tu, bali ni wa kindugu wa kihistoria uliodumu kwa miaka mingi hata kabla ya ukoloni. Amesema kufanana kwa mila, tamaduni na historia ni ushahidi wa undugu huo wa karibu unaowaunganisha wananchi wa mataifa haya mawili. Akizungumza baada ya mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aliyefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania, Rais Samia alieleza kuwa nchi hizi mbili zimeendelea kushirikiana kwa karibu katika ngazi za kikanda na kimataifa. Ushirikiano huo unajumuisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU), pamoja na Umoja wa Mataifa (UN). Katika nyanja ya uchumi, Rais Samia alibainisha kuwa biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekua kwa kiwango kikubwa, ikifikia thamani ya shilingi bilioni 644 katika mwaka uliopita. Aidha, kuanzia mwaka 1997 hadi Machi mwaka huu, Tanzania imesajili miradi 42 ya…