TADB YAWAWEZESHA WAFUGAJI WADOGO ZAIDI YA 92, 000 KUPITIA MRADI WA MAZIWA WA TI3P
TADB YAWAWEZESHA WAFUGAJI WADOGO ZAIDI YA 92, 000 KUPITIA MRADI WA MAZIWA WA TI3P
Jumla ya wafugaji wadogo 92,831 na wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwawa Tanzania Bara na Visiwani-Zanzibar wamenufaika na Mradi Shirikishi waWasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) tangu ulipoanzishwa mwezi Machi mwaka 2022, ambapo asilimia 30 ya wanufaika hao ni wanawake. Mradi huo wa miaka minne unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya KilimoTanzania - TADB pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ukitekelezwakwa kushirikiana na Heifer International, Land O’Lakes Venture37 pamoja naTanager. Akiongea wakati wa Maonesho ya Wiki ya Maziwa Mkoani Iringa, Mratibu waMradi wa TI3P, Joseph Mabula amesema mradi huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ndogo ya maziwa ilikuongeza uzalishaji, na kuboresha kipato cha wafugaji wadogo wa maziwa nchinihuku akiishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. SamiaSuluhu Hassan kwa kuipa uzito mkubwa sekta ndogo ya maziwa. Mabula amesema tangu kuanza kwake, mradi umewezesha utole…