SMZ KUILINDA AMANI KWA GHARAMA ZOTE
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesisitiza msimamo wake wa kuendelea kuilinda amani na utulivu wa visiwa hivyo kwa gharama zote, huku ikiwatahadharisha wanasiasa kuacha tabia ya kuwashawishi vijana kujiingiza katika vurugu kwa ajili ya maslahi yao binafsi ya kisiasa. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Amesema kuwa Zanzibar imeshuhudia utulivu mkubwa uliowezesha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka jana kufanyika kwa amani na usalama, jambo ambalo limejipatia sifa kupitia ripoti za waangalizi wa ndani na nje ya nchi. Amebainisha kuwa wananchi wa Zanzibar wamechoshwa na vurugu za kisiasa zinazowanufaisha viongozi wenye uchu wa madaraka, hivyo Serikali ya Awamu ya Nane imeelekeza nguvu zake zote katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 kupitia miradi ya kimkakati. Abdulla amewahakikis…