SERIKALI YATAKA WAZAZI WASIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU
SERIKALI YATAKA WAZAZI WASIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU
SERIKALI imewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu na badala yake kuwapeleka kupata matibabu, elimu na huduma nyingine za msingi ili waweze kutimiza ndoto zao kama watoto wengine katika jamii. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, Mei 30, 2026 alipotembelea Kituo cha Makazi ya Watoto Wenye Ulemavu cha Mlali kilichopo Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma. Akizungumza na wananchi, wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu, Mhe.Nderiananga amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma, hususan watu wenye ulemavu. Amesema kundi hilo lina haki sawa na makundi mengine katika kupata elimu, matibabu, ulinzi na fursa mbalimbali za maendeleo. Pia, amewataka wazazi kuacha kuona aibu au kuficha watoto wenye ulemavu, akisisitiza kuwa watoto hao wana vipaji, uwezo…