Posts

SERIKALI YAKABIDHI MITAJI KWA VIJANA 47 WA BBT- UVUVI KAGERA

SERIKALI YAKABIDHI MITAJI KWA VIJANA 47 WA BBT- UVUVI KAGERA
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Erasto Sima ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, amesema Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia Sekta ya Uvuvi ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini. Mhe. Sima  amesema hayo Mei 9, 2026 katika hafla ya kukabidhi mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana 47 walionufaika na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT–Uvuvi) iliyofanyika Katika Mwalo wa Bilolo Kemondo  Bukoba.  “Programu hii inalenga kutoa mafunzo kwa vitendo pamoja na mitaji ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuwa wawekezaji katika Sekta ya Uvuvi,” amesema Mhe. Sima Aidha, Mhe. Sima amesema kuwa hafla hiyo ni mwendelezo wa ugawaji wa mitaji uliozinduliwa Machi 7, 2026 katika eneo la FETA Nyegezi mkoani Mwanza, ambapo vijana 55 walikabidhiwa pembejeo mbalimbali za ufugaji wa samaki kwa vizimba. Mhe. Sima amewataka wanufaika hao kutumia fursa waliyopewa kwa uwajibikaji, nidhamu na uadilifu ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta matokeo chanya kwao bina…