Serikali yaitaka TBA kuingia ubia na sekta binafsi na kutekeleza miradi mingi zaidi

Serikali yaitaka TBA kuingia ubia na sekta binafsi na kutekeleza miradi mingi zaidi
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV SERIKALI Kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) inatekeleza mradi nyumba za makazi kwa watumishi wa Umma vijana ‘Temeke Kota’ jijini Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi Bilioni 21 ikiwa ni sehemu ya kutafuta suluhu ya makazi kwa vijana walioajiriwa katika ofisi za Umma na kufuatiwa na miradi itakayowalenga vijana wasio watumishi wa Umma. Akizungumza leo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa vijana watumishi wa Umma wa Temeke Kota Jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema; mradi huo wa Nyumba za gharama nafuu una nyumba zitakazobeba familia 144 ambapo nyumba 72 ni chumba kimoja na sebule na choo (studio apartment,) na nyumba 72 ni vyumba viwili pamoja na sebule mahususi kwa wenye familia ndogo. Waziri Ulega amesema,Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan suluhu imejizatiti kutafuta suluhu ya nyumba za makazi kwa gharama nafuu na TBA wamekuwa wakifanya jitihada za kina katika kutatua chan…