SERIKALI YAHIMIZA ULINZI WA AMANI KAMA NGAO YA MAENDELEO YA TAIFA
SERIKALI YAHIMIZA ULINZI WA AMANI KAMA NGAO YA MAENDELEO YA TAIFA
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewahimiza Watanzania kulinda na kutunza amani kwa wivu mkubwa ili kuwezesha nchi kufikia malengo yake ya kimaendeleo. Akizungumza na waandishi pamoja na maofisa habari mkoani Njombe, Msigwa alisisitiza kuwa hakuna nchi duniani iliyowahi kupata maendeleo ya kweli ikiwa wananchi wake wanavurugana na kugombana kila kukicha. Alieleza kuwa ni jukumu la kila mwananchi kukataa hamasa zozote zinazoashiria fujo na vurugu, akionya kuwa mabeberu bado hawajalala na mara nyingi hutumia baadhi ya Watanzania miongoni mwetu kufanikisha ajenda zao za kuvuruga nchi. Msigwa alifafanua kuwa ni vigumu kupiga hatua za kiuchumi ikiwa jamii itajikita kwenye maandamano ya kila siku na uharibifu wa miundombinu ambayo ndiyo uti wa mgongo wa biashara na usafirishaji. Alitolea mfano wa wakulima wa maparachichi mkoani Njombe ambao wanategemea utulivu ili kuzalisha, akibainisha kuwa vitendo vya kuchoma bandari au viwanja vya ndege vinavyohamasishwa na baadhi ya watu kwenye mit…