SERIKALI YAHAMASISHA WANANCHI KULINDA HAKI NA USTAWI WA PUNDA.
SERIKALI YAHAMASISHA WANANCHI KULINDA HAKI NA USTAWI WA PUNDA.
Serikali imeendelea kuweka nguvu katika kulinda haki na ustawi wa mnyama kazi punda kutokana na umuhimu wake kwa jamii katika kusaidia shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato kwa wananchi. Serikali imezitaka mamlaka zote kuhakikisha zinasimamia Sheria ya Wanyama, ikiwemo kulinda punda dhidi ya ukatili na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria hizo, aidha imehimiza wananchi kuhakikisha wanyama hao wanapatiwa chakula, matibabu pamoja na kutobughudhiwa. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita katika Maadhimisho ya Siku ya Punda Duniani yaliyofanyika kitaifa katika Mtaa wa Mgusu, Manispaa ya Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakipuuzia thamani ya punda huku wakimtendea ukatili mnyama huyo. Maadhimisho hayo yameratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la INADES-Formation Tanzania, ASPA pamoja na mashirika mengine kwa ufadhili wa Brooke East Africa. Komba amesema kutoweka kwa punda kutasababisha athari kub…