Serikali Kuzindua Mpango Mkakati wa Mazingira 2026–2030

Serikali Kuzindua Mpango Mkakati wa Mazingira 2026–2030
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yatayofanyika  Juni 5 mwaka huu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwa na Wakuu wa Taasisi zilizo kuwa Chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yatayofanyika  Juni 5 mwaka huu. Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema inatarajia kuzindua mpango mkakati maalum wa mazingira utakaotekelezwa kuanzia mwaka 2026 hadi 2030 katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini. Hayo ameyasema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu was Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni wakati akitangaza Siku ya Mazingira Duniani itayofanyika Juni 5 Mwaka huu. Masauni, amesema mkakati utaozinduliwa unalenga kushughulikia kwa kina changamoto mbalimbali za kimazingira, ikiwe…