SANGU: TUTAENZI MCHANGO WA WAKILI SWAI

SANGU: TUTAENZI MCHANGO WA WAKILI SWAI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu leo ameongoza watumishi, mawakili na wananchi kumuaga aliyekuwa mtumishi wa Ofisi hiyo, marehemu Wakili Msomi Charles Boaz Swai aliyefariki jana jijini Dodoma. Tukio hilo la Ibada na kisha kutoa heshima za ilifanyika nyumbani kwa marehemu eneo Chaduru Mei 29, 2026 ambapo Waziri Sangu alieleza kuwa mchango wa Marehemu Wakili Swai utaendelea kukumbukwa na kwamba Ofisi yake inamshukuru Mungu kwa maisha ya Wakili Swai kutokana utumishi wake . Akieleza kuhusu namna Marehemu Swai alivyotoa mchango wake, Waziri Sangu aliwaeleza waombolezaji kuwa ni wiki moja imepita alifanya kazi ofisini kwake na Wakili Swai ambapo walikubaliana kuendelea kukamilisha jambo hilo lakini ghafla Mwenyezi Mungu amemchukua na kuwataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kuenzi mchango wa marehemu Wakili Swai. "Marehemu Swai ni wiki tu imepita nilikuwa naye ofisini kwangu tukijadili utekelezaji wa kazi ambapo ushauri wake …