PUGU KAZIMZUMBWI: HAZINA YA UTALII INAYOHIFADHI HISTORIA NA BIOANUAI
PUGU KAZIMZUMBWI: HAZINA YA UTALII INAYOHIFADHI HISTORIA NA BIOANUAI
-Wahifadhi wa Sao Hill wavutiwa na mafanikio ya utalii ikolojia, watakiwa kuhamasisha kura za Tuzo za Kimataifa za Utalii Na Mwandishi Wetu, Pwani Hifadhi ya Msitu wa Asili ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani imeendelea kujidhihirisha kuwa moja ya hazina kubwa za utalii wa ikolojia nchini baada ya kuvutia wahifadhi kutoka Shamba la Miti Sao Hill waliotembelea eneo hilo kujifunza mbinu za uhifadhi, usimamizi wa bioanuai na maendeleo ya utalii endelevu. Ziara hiyo imekuja wakati Tanzania ikiendelea kuimarisha juhudi za kuhifadhi rasilimali za misitu na kuendeleza utalii wa asili kama sehemu ya kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa, huku Pugu Kazimzumbwi ikitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kuhifadhi urithi wa kihistoria na mazingira ya kipekee karibu na Jiji la Dar es Salaam. Wakati wa ziara hiyo, wahifadhi hao walitembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo misitu ya asili yenye bioanuai adimu, njia za utalii wa kutembea msituni, mae…