PROF. SHEMDOE ASISITIZA SUALA LA USAFI LIWE AJENDA YA KUDUMU KATIKA VIKAO VYOTE NGAZI ZA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

PROF. SHEMDOE ASISITIZA SUALA LA USAFI LIWE AJENDA YA KUDUMU KATIKA VIKAO VYOTE NGAZI ZA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA
Na OWM – TAMISEMI, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewasisitiza washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Afua ya Uthibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Miji, kuhakikisha suala usafi wa mazingira linakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vitakavyofanyika katika ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuwezesha miji na majiji nchini kuwa masafi. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo Mei 12, 2026 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Mwaka wa Tathmini ya Afua ya Uthibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Miji, unaofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Jiji- Mtumba, unaohudhuriwa na Maafisa Afya wa Mikoa, Maafisa Afya wa Halmashauri na Maafisa Mazingira wa Halmashauri. “Nasisitiza suala la usafi wa mazingira liwe ajenda ya vikao vyenu. Vikao vya Kamati za Ushauri za Mikoa, Kamati za Ushauri za Wilaya, Kamati za Maendeleo za Kata, Mabaraza ya Madiwani, Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na vya ALAT nga…