ORXY YAZINDUA KITUO KIPYA CHA MAFUTA WILAYANI KARATU,SERIKALI YATOA NENO

ORXY YAZINDUA KITUO KIPYA CHA MAFUTA WILAYANI KARATU,SERIKALI YATOA NENO
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Karatu SERIKALI imesema itaendelea kuwalinda wawekezaji wa ndani pamoja na kuunga mkono uwekezaji wowote unaofanywa na wawekezaji hao kwa lengo la kutoa huduma za kijamii. Hayo yameelezwa leo 29 Mei 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Lameck Karanga katika hafla ya uzinduzi wa kituo kipya ya mafuta cha Orxy kitakachokuwa kikiendeshwa chini ya kampuni ya halyaz. DC Karanga amesema ujenzi wa kituo hicho cha mafuta ni muendelezo wa maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanajengewa mazingira mazuri Ili waweze kufanya biashara. Amesema Karatu ndio lango kuu la utalii hivyo ujio wa kituo hicho kutasaidia wasafirishaji kupata nishati ya mafuta kwa urahisi na uhakika kwa kuwa bidhaa za kampuni hiyo zinaaminika katika ukanda wa Afrika na duniani kote. "Kwa niaba ya Wilaya niwapongeze sana kwa uwekezaji huu, mbali ya kutuletea kituo bora lakini mmeanza na kutengeneza mazingira hasa ya bustani nzuri hapo mbele ya kituo chenu, hii inaony…