OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YATOA WITO WA UTAWALA BORA KUIMARISHA UWEKEZAJI WA UMMA
OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YATOA WITO WA UTAWALA BORA KUIMARISHA UWEKEZAJI WA UMMA
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Chacha Marigiri, akiwasilisha mada kuhusu ‘Utawala bora katika mashirika ya Umma na Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina’ katika Mkutano wa Jukwaa la Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma Zanzibar uliofanyika tarehe 24 Mei 2026 katika hoteli ya Golden Tulip Airport. ** Zanzibar. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio ya taasisi na mashirika ya umma nchini unategemea kwa kiwango kikubwa uimara wa mifumo ya utawala bora, uwajibikaji na uongozi wenye maono yanayolenga matokeo. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Chacha Marigiri, alipowasilisha mada kuhusu ‘Utawala bora katika mashirika ya Umma na Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina’ katika Mkutano wa Jukwaa la Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma Zanzibar uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Airport. Katika wasilisho lake Jumapili, Mei 24, 2026…