MPANGO MKAKATI WA MAGEUZI KWA MAZINGIRA ENDELEVU KUZINDULIWA

MPANGO MKAKATI WA MAGEUZI KWA MAZINGIRA ENDELEVU KUZINDULIWA
SERIKALI inatarajia kuzindua Mpango Mkakati wa Mageuzi kwa Mazingira Endelevu wa mwaka 2026 hadi 2030 utakaolenga kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamadi Yussuf Masauni alisema jijini Dar es Salaam kuwa mpango huo ni sehemu ya mageuzi mapana ya sekta ya mazingira yanayolenga kushughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo usimamizi duni wa taka ngumu mijini, matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali pamoja na uharibifu wa mazingira. Masauni alisema mkakati huo utakuwa mfumo wa kitaifa wa mwongozo utakaoratibu hatua za kimazingira kwa kipindi cha miaka mitano, ukiweka mkazo katika uendelevu, ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na mageuzi ya uchumi wa kijani. Alisema utekelezaji wa mpango huo utahakikisha uratibu wa pamoja katika sekta muhimu za uchumi zikiwemo kilimo, nishati, viwanda pamoja na maendeleo ya mijini ili kuhakikisha agenda ya mazi…