MKURUGENZI MKUU VETA AWATAKA WAKUFUNZI 25 WALIOPO NCHINI FINLAND KUWA CHACHU YA MABAILIKO
MKURUGENZI MKUU VETA AWATAKA WAKUFUNZI 25 WALIOPO NCHINI FINLAND KUWA CHACHU YA MABAILIKO Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amefanya ziara katika chuo cha REDUEdu kilichopo Rovaniemi nchini Finland ili kujionea maendeleo ya wakufunzi 25 wanaopata mafunzo ya ujuzi wa teknolojia zinazohitajika katika Uchimbaji na Ukuzaji Mnyororo wa Thamani wa Madini chuoni hapo. Katika ziara yake chuoni hapo aliambatana na baadhi ya viongozi wa menejimenti ya VETA Makoa Makuu, jana tarehe 22 Mei 2026 CPA Kasore, amezungumza na wakufunzi hao na kuwataka pindi watakapo hitimu mafunzo yao na kurejea nchini kuhakikisha wanaleta mabadiliko chanya katika taasisi na taifa. “Kuja kwetu hapa ni kutaka kuona kile tunachokisimamia watu wetu wanakipata kupitia huu mradi. Ndio maana hata leo tulikuwa na majadiliano na wenzetu REDUEdu na GTK kuona mpangilio wa vipindi ukoje na kwa kiasi gani umetekelezwa na wapi pa kufanya maboresho” amesema Kasore. Aidha CPA Kasore amewataka wakufunzi hao kupita katika karakana zilizopo chuoni hapo ili kujionea hali ya mpangilio wa vifaa vya kujifunzia lakini pia …