MIAKA 18 BAADAYE: JK AKUTANA TENA NA CATHERINE, BINTI ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO AKIWA NA MIAKA MINNE

MIAKA 18 BAADAYE: JK AKUTANA TENA NA CATHERINE, BINTI ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO AKIWA NA MIAKA MINNE
RAIS  mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Mei 29, 2026 amekutana tena na Bi. Catherine P. Conrad Minja, aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio akiwa na umri wa miaka minne katika taasisi ya Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) miaka 18 iliyopita. Wakati huo madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI walikuwa wakitumia majengo ya MOI kabla jengo lao halijakamilika. Mara ya kwanza wawili hao walikutana Novemba 14, 2008 wakati Dkt. Kikwete akiwa Rais alipokwenda kumjulia hali Catherine hapo MOI baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo. Wakati huo Catherine alikuwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika taasisi hiyo. Miaka 18 baadaye, Catherine amekua na sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Kairuki jijini Dar es salaam. Alifika ofisini kwa Rais Mstaafu kumsabahi na kumshukuru kwa mchango wake katika kuanzisha na kuimarisha huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini. Dkt. Kikwete alimpongeza Cath…