MDEMU AWATAKA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUDUMISHA MALEZI BORA

MDEMU AWATAKA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUDUMISHA MALEZI BORA
Na Saidi Saidi, WMJJWM – Iringa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Felister Mdemu, amewataka wanawake kushirikiana katika kujikwamua kiuchumi huku wakiendelea kuthamini familia, malezi bora, kuwaheshimu waume zao na kuhakikisha watoto wanapata malezi yenye maadili mema. Mdemu amesema hayo mkoani Iringa, wakati wa mafunzo ya mwongozo wa uanzishwaji na uwezeshaji wa majukwaa ya wanawake kiuchumi yaliyofanyika katika Kijiji cha Kipaduka, Kata ya Uhambingeto, wilayani Kilolo. Mafunzo hayo yalihusisha madiwani pamoja na viongozi wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka kata mbalimbali za mkoa huo. Akizungumzia umuhimu wa majukwaa hayo, Mdemu amesema ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia elimu ya fedha, ujasiriamali, matumizi ya teknolojia pamoja na upatikanaji wa mikopo na masoko. Aidha, amesisitiza umuhimu wa wanawake kupata taarifa sahihi, …