MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026 MKOA WA DODOMA

Dodoma, Mei 29, 2026 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu M. Kazungu anautaarifu Umma   kuwa, Mkoa unatarajia kuanza mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 31/05/2026, ambapo utapokelewa rasmi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mtera,Wilaya ya Mpwapwa, kabla ya kuanza mbio zake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma. Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya zote 7 na Halmashauri 8 za Mkoa huu, kwa umbali wa kilomita 1,595.3 huku miradi 54 ya maendeleo ikipitiwa, ambapo miradi 21 itawekewa mawe ya msingi, miradi 2 itafunguliwa rasmi, miradi 20 itazinduliwa, na miradi 11 itakaguliwa. Miradi hiyo yote ina thamani ya shilingi 23,243,056,418.58 ambapo vyanzo vya fedha hizo ni; Serikali Kuu shilingi 10,605,347,151.67, mapato ya ndani ya Halmashauri   shilingi 4,103,038,865.71, michango ya Wananchi shilingi 1,841,600,000.00 pamoja na Wafadhili na Wadau waliotoa shilingi 6,693,070,401.20. Ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Dodoma 2026 ni kama ifuatavyo 31/05/2026 – Halmashauri ya W…