MATIVILA AAGIZA WAKANDARASI KUZINGATIA UBORA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI
MATIVILA AAGIZA WAKANDARASI KUZINGATIA UBORA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM- TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali chini ya Mradi wa TACTIC kuzingatia viwango vya ubora vilivyoainishwa katika mikataba yao. Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo Mei 29,2026 wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya miundombinu inayotekelezwa na TACTIC katika mkoa wa Mara, ambapo amesisitiza kuwa ubora wa kazi ni jambo lisilopaswa kufanyiwa mzaha. “Katika ziara hii, moja ya mambo muhimu tunayoyaangalia ni ubora wa miradi kwa kuzingatia maelezo yaliyopo kwenye mikataba, hivyo wakandarasi wote mnapaswa kuhakikisha mnatekeleza kazi kwa viwango vilivyokubaliwa,” amesema Mhandisi Mativila. Ameeleza kuwa wakandarasi wanaposaini mikataba ya utekelezaji wa miradi, wanakuwa wamekubali kutekeleza kazi kwa ubora unaotakiwa, hivyo ni wajibu wao kujisimamia na kuhakikisha wanazingatia masharti yote ya mikataba bila kushurutish…