MAKAA YA MAWE YA RUVUMA YAFUNGUA MASOKO YA AFRIKA NA ASIA
MAKAA YA MAWE YA RUVUMA YAFUNGUA MASOKO YA AFRIKA NA ASIA
Mkoa wa Ruvuma umeendelea kujizolea umaarufu katika sekta ya madini baada ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika wilaya za Mbinga, Songea na Nyasa kufungua masoko katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia, huku zaidi ya tani milioni 3.6 zikizalishwa mwaka 2024/2025 na kuchochea ajira, biashara na matumizi ya nishati safi. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi amesema shughuli za utafiti, uchimbaji na uchakataji wa makaa ya mawe zinazofanywa na makampuni pamoja na wadau mbalimbali zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla. Amesema makaa hayo yenye ubora wa hali ya juu yanatumika katika viwanda vya saruji, usafishaji wa vyuma na shughuli nyingine za viwandani, huku sehemu ya uzalishaji ikipelekwa katika masoko ya Kenya, Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). “Migodi ya makaa ya mawe ya Ruvuma imeendelea kuvutia wawekezaji kutokana na ubora wa madini hayo, hali iliyosaidia kufungua masoko mapya katika …