MAHAKAMANI KWA KUTOTOA RISITI YA EFD YA CHIPS KUKU

MAHAKAMANI KWA KUTOTOA RISITI YA EFD YA CHIPS KUKU
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imewahukumu raia wa China XU Fuyu (39) na mfanyakazi wake wa mgahawa wa Kibonge, Blandina Mwalutola (24) wamehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni  sita kwa kushindwa kutoa risiti ya kielektroniki, baada ya kutoa huduma ya chipsi kuku, sahani ya baga, sahani ya wali na vinywaji. Washtakiwa hao walishtakiwa Kinyume na Kifungu cha 97(1)(b) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi [Sura ya 438 Toleo la 2023], kikisomwa pamoja na Vifungu vya 96 na 97 vya Sheria ya Fedha Na. 6 ya mwaka 2024. Pia imedaiwa walikamatwa, wakati maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakiwa katika utafiti na upelelezi kuhusiana na utoaji wa risiti za kielektroniki. Ambapo imedaiwa waliagiza chakula na vinywaji ila walipewa risiti za mkono. Hukumu hiyo, imetolewa leo Mei 8, 2026 na Hakimu Mwandamizi Mohamed Burhani, baada ya washtakiwa kukiri mashtaka mawili kushindwa kutoa risiti za kielektroniki kinyume na sheria za kodi. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Burhani amesema kesi kama hizo lazima adha…