KUIMARISHWA KWA MIFUMO YA USIMAMIZI WA MAAFA TANZANIA KWATOA SOMO MAPAI MSUMBIJI

KUIMARISHWA KWA MIFUMO YA USIMAMIZI WA MAAFA TANZANIA KWATOA SOMO MAPAI MSUMBIJI
Na, Mwandishi wetu, Mapai – Msumbiji TANZANIA imeendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha udhibiti wa maafa unaanzia ngazi ya chini ya jamii, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika tahadhari, maandalizi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, walipotembelea Wilaya ya Mapai iliyoko mkoa wa Gaza Nchini Msumbiji ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema za kukabiliana na majanga. Amesema moja ya mambo makubwa yakujivunia ni namna mifumo ya usimamizi wa maafa ilivyoimarika kuanzia ngazi ya chini jambo linalosaidia kuongeza ufanisi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea. Aidha, akieleza faida ya ziara hiyo Wilayani Mapai ni kuchukua uzoefu wa namna ya kuongeza tija katika eneo la kurejesha hali na kukabiliana na maafa kwa kuwa na miradi ya kuto…