KISWAGA APONGEZA UTEUZI WA EMANUELA KAGANDA ISIMANI
NA DENIS MLOWE, IRINGA MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, Festo Shem Kiswaga, ambaye anatoka katika eneo la Iringa Vijijini, leo amezungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa ndefu kuhusu mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Isimani. Akizungumza Kiswaga alisema kuwa amehudumu kama mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa takribani miaka kumi na tano, na pia amewahi kuwa mtendaji wa serikali hadi ngazi ya wilaya, uzoefu ambao anasema umemjengea uelewa mpana wa taratibu za chama na serikali. Kiswaga alianza kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa viongozi wa chama ngazi ya wilaya, akiwemo mwenyekiti wa CCM wilaya, kamati ya siasa ya wilaya, na katibu wa chama, kwa usimamizi wao makini katika zoezi la kura za maoni. Pia aliwapongeza viongozi wa ngazi ya mkoa kwa weledi na uwazi waliouonyesha katika usimamizi wa mchakato, akiwataja viongozi hao kama sehemu muhimu ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama. Aidha, aliwashukuru viongozi wa taifa akiw…