KAMPUNI YA CRJE YAWAKUTANISHA WATOTO WA KICHINA NA TANZANIA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UTAMADUNI SIKU YA MTOTO
KAMPUNI YA CRJE YAWAKUTANISHA WATOTO WA KICHINA NA TANZANIA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UTAMADUNI SIKU YA MTOTO
Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM– Kampuni ya CRJE (East Africa) Ltd imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto kwa kuwakutanisha pamoja watoto wa Kitanzania na wenzao wa Kichina ili waweze kupata fursa ya kuweza kubadilishana utamaduni Kwa ajiri ya kuendelea kukuza urafiki mkubwa uliopo kati ya China na Tanzania. Ubadilishanaji wa ujuzi wa kitamaduni kati ya watoto wa China na Tanzania unaendelea kukua na kushamiri kupitia programu mbalimbali za kitaasisi na shule zinazowaweka pamoja watoto wa mataifa haya mawili. Zaidi ya watoto thelathini wa wafanyakazi wa Kampuni ya CRJE wa Kichina na Kitanzania pamoja na wanafunzi kutoka shule za Dar es Salaam na Dodoma walishiriki Siku hiyo ambapo Taifa la China huazimisha siku ya mtoto Duniani Juni 1. Tukio Hilo lilibebwa na kauli mbiu ya “Daraja la Vijana Linalea Watoto, Vijana Waanzilishi Wajenga Mustakabali” Walimu wa shule zilizoshiriki walibainisha kuwa wanafunzi mara nyingi hujifunza kuhusu nchi nyingine kupitia vitabu. Matukio kama haya huwafanya …