JKCI YAWAGUSA WANANCHI NJOMBE KUPITIA KAMPENI YA “JUA NAMBA ZAKO”

JKCI YAWAGUSA WANANCHI NJOMBE KUPITIA KAMPENI YA “JUA NAMBA ZAKO”
Na Mwandishi Maalumu – Njombe 9/5/2026 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imewahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kupitia kampeni ya “Jua Namba Zako” ili kubaini mapema vihatarishi vya magonjwa ya moyo na kupata matibabu kwa wakati. Rai hiyo imetolewa leo na Daktari wa Taasisi hiyo Samweli Mbilinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma za upimaji wa moyo zinazotolewa na JKCI kwenye Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kinachofanyika katika Hoteli ya Agreement iliyopo mjini Njombe. Dkt. Mbilinyi alisema wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu magonjwa ya moyo jambo linalosababisha baadhi yao kuishi na matatizo hayo bila kujitambua hadi wanapofika hospitalini wakiwa na matatizo mengine. Alitoa mfano wa mgonjwa aliyefika katika upimaji huo ambao huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbali zinatolewa kwajili ya matatizo ya miguu lakini baada ya kupimwa alibainika kuwa na shinikizo kubwa …