Hatari Isiyoonekana: Teknolojia Mpya ya Tanzania Yaanza vita dhidi ya Sumu Kuvu

Hatari Isiyoonekana: Teknolojia Mpya ya Tanzania Yaanza vita dhidi ya Sumu Kuvu
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV KATIKA ghala moja la kuhifadhi mazao nchini Tanzania, mfumo wa kielektroniki unapiga kengele. Dakika chache baadaye, ujumbe unaingia kwenye simu ya msimamizi wa ghala ukionya kuwa kiwango cha joto na unyevunyevu kimeanza kufikia mazingira yanayoweza kuzalisha sumu kuvu kwenye mahindi yaliyohifadhiwa. Onyo hilo halihusu moto wala uvamizi wa wahalifu. Linaashiria uwepo wa mazingira yanayoweza kuchochea kuzalishwa kwa sumu kuvu kwenye mazao ya chakula. Ingawa mazao kama mahindi, mtama na karanga ni sehemu ya chakula cha kila siku kwa mamilioni ya Watanzania, si wananchi wote wanaofahamu kuwa yanaweza kuwa chanzo cha hatari kubwa kiafya yanapoathiriwa na sumu kuvu. Unapuzungumzia sumu kuvu katika mazao kama vile mtama, mahindi, na karanga, siyo Wananchi wote wanafamu kuwa sumu kuvu inaweza kuleta madhara kwa binadamu na mifugo na hatimaye kusababisha kansa ya ini. Sumu kuvu ni aina ya sumu inayotengenezwa na kuvu au fangasi wanaoota kwenye mazao mbalimbali hasa …