GPE, EP4R WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU BUSWELU

GPE, EP4R WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU BUSWELU
Ujumbe wa wadau wa maendeleo ya elimu ukiwemo Global Partnership for Education (GPE) pamoja na Education Program for Results (EP4R) ukiongozwa na Morten Sigsgaard Mratibu wa Ushirika wa Nchi (GPE) umeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa katika Shule ya Msingi na Sekondari Buswelu, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo Mei 11, 2026, Morten amesema miradi hiyo imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, hususan kwa wanafunzi wa elimu jumuishi. Katika Shule ya Msingi Buswelu, inayohudumia wanafunzi 1,211 wakiwemo 176 wenye mahitaji maalumu, imefanikiwa kujenga bweni la wasichana wenye mahitaji maalumu kupitia ufadhili wa Serikali na GPE-LANES II. Mradi huo9 umewezesha wanafunzi 80 kupata makazi salama ya bweni, huku huduma za bweni zikianza rasmi Mei 8, 2026 baada ya Serikali kuanza kutoa fedha za chakula. Aidha, walimu na wanafunzi wameeleza mabadiliko chanya yaliyotokana na miradi hiyo, wak…