DKT. NCHEMBA: BARABARA YA MCHEPUO IRINGA KUCHOCHEA UCHUMI

DKT. NCHEMBA: BARABARA YA MCHEPUO IRINGA KUCHOCHEA UCHUMI
📌Asema mradi huo utafungua fursa mpya za uchumi na kupunguza msongamano wa magari mjini Iringa 📌Aagiza malipo ya vibarua yafanyike kwa wakati  Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya miundombinu ili kuboresha usafiri, kuongeza ufanisi wa uchukuzi na kufungua fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi nchini. Amesema hayo leo Jumamosi, Mei 23, 2026 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mchepuo ya Mji wa Iringa (Iringa Municipal Bypass) yenye urefu wa kilomita 7.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Iringa. “Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla. Itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuongeza biashara na kuchochea ukuaji wa mji wa Iringa,” amesema Dkt. Nchemba. Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya barabara nchini kwa lengo la kuima…