DKT. MWIGULU: WEZI WA FEDHA ZA UMMA WASIHAMISHWE, WAKAMATWE MARA MOJA
DKT. MWIGULU: WEZI WA FEDHA ZA UMMA WASIHAMISHWE, WAKAMATWE MARA MOJA
Na Janeth Raphael -MichuziTv Singida Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wote wa umma watakaobainika kuhusika na ubadhirifu wa fedha za Serikali, akisisitiza kuwa tabia ya kuwahamisha badala ya kuwakamata imekuwa ikichangia kuendelea kwa vitendo vya wizi katika maeneo mbalimbali nchini. Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Mei 31, 2026 wakati akizungumza na wananchi wa Itigi mkoani Singida, ambapo ameeleza kuwa Serikali haitavumilia watumishi wanaotumia nafasi zao vibaya kwa kuiba mali na fedha za umma zilizotokana na kodi za wananchi. Amesema watumishi wanaobainika kufanya ubadhirifu hawapaswi kuhamishwa kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine kwani hatua hiyo haina tija, badala yake huwapa nafasi ya kuendelea kufanya vitendo hivyo katika maeneo mapya wanayopelekwa. “Mwizi wala msimuhamishe. Mkishamhamisha anaenda kuiba na huko. Wale ambao walishahamishwa, kule walikopelekwa RPC wa huko aw…