DKT. MWIGULU AAGIZA WALIOIBA MILIONI 500 MANYONI KUKAMATWA

*Aagiza watumishi waliohusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 Manyoni wakamatwe na fedha zirudishwe * Akemea rushwa, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka * Aonya viongozi wanaowaza vyeo badala ya kutatua changamoto za wananchi WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni watafutwe popote walipo, wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu huku fedha hizo zikirejeshwa serikalini. “Wamechota fedha za wananchi. Watafutwe hata ambao walishahamishwa, popote walipo wakamatwe, wawekwe ndani na fedha za Serikali zirudi. Hii si fedha ya mtu binafsi, ni fedha ya wananchi,” alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni katika Viwanja vya Tambukareli mkoani Singida akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto z…