DKT. AKWILAPO KUWAUNGA MKONO VIJANA WANAOTENGENEZA SAMANI MASASI

DKT. AKWILAPO KUWAUNGA MKONO VIJANA WANAOTENGENEZA SAMANI MASASI
Na Munir Shemweta, MASASI Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameahidi kukiunga mkono kikundi cha vijana cha UBINAKI kinachojishughulisha na mradi wa utengemezaji samani za majumbani na ofisini. Mradi wa vijana wa UBINAKI unatokana na mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kwa makundi ya vijana, wanawake pamoja na watu wenye walemavu ambapo vijana hao wa Masasi wameonesha ubunifu mkubwa pamoja na matumizi sahihi ya fedha walizopatiwa kwa kuanzisha shughuli yenye tija kwao na kwa jamii inayowazunguka. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa vijana wa UBINAKI wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa jana katika halmashauri ya Mji Masasi Dkt Akwilapo amewapongeza vijana hao kwa kuungana, kufanya kazi pamoja sambamba na kujitegemea katika kuendesha shughuli za kujitafutia kipato. ‘’Hawa ni mfano wa kuigwa na ningependa vijana wengine wote waige mfano wa vijana hawa na mimi hawa nitawaunga mkono’’ ame…