DK. SAJAD HABIB RAI: MBUNIFU WA MFUMO WA KUDHIBITI UKWEPAJI KODI KATIKA SEKTA YA MAFUTA
DK. SAJAD HABIB RAI: MBUNIFU WA MFUMO WA KUDHIBITI UKWEPAJI KODI KATIKA SEKTA YA MAFUTA
*Kinara wa Mageuzi Sekta ya Mafuta *Ampongeza Rais Samia kwa Uchapakazi, Asema Tanzania Itashinda Changamoto ya Mafuta Na Mwandishi Wetu KATIKA ulimwengu wa biashara na uchumi wa kisasa, viongozi wachache huweza kuunganisha utaalamu, ubunifu, uzalendo na uwezo wa kuleta matokeo yanayoonekana ndani ya muda mfupi. Tanzania imebahatika kuwa na baadhi ya viongozi wa aina hiyo ambao kupitia maarifa yao wameendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa. Miongoni mwao ni Dk. Sajad Habib Rai, mtaalamu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya mafuta, usafirishaji, manunuzi, teknolojia ya habari na usimamizi wa biashara. Kupitia nafasi yake kama Meneja Mkazi wa Mansoor Industries Limited, Dk. Sajad ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia operesheni za biashara huku akihakikisha kampuni inaendelea kukua na wakati huo huo kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza mapato ya taifa. Safari ya Mafanikio Dk. Sajad, mwenye umri wa miaka 47, alianza safari yake ya kitaaluma kwa misingi ya n…