Diwani Tousif atatua kero kata ya kisutu
Na MWANDISHI WETU DIWANI wa Kata ya kisutu, jijini Dar es Salaam, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM) , Tousif Bhojani, ameibua shangwe kwa wakazi wa eneo hilo baada ya kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zilizo kuwa zikiwakabili. Bhojani ametatua karo mbalimbali za wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika katika Viwanja vya Soko la Kisutu, ambao ulihusisha pia wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za serikali ambao walizitolea majibu baadhi ya changamoto. Kero hizo ni pamoja na ukosefu wa kisima cha maji katika Soko la Baba na Mamalishe Kisutu, kuvuja kwa paa la soko hilo na ukosefu wa vifaa vya zimamoto. Changamoto zingine ni maegesho, kero ya kamata kamata ya 'wrong parking', ulinzi na usalama, mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri na utirikaji wa maji taka. Katika kutatua changamoto ya Soko la Mama na Baba Lishe Kisutu kutokuwa na kisima, Diwani Bhojani aliwasiliana kwa simu papo hapo na Spika wa Bunge ambaye pia ni …