DIWANI KATA YA ZINGIZIWA ATOA MSAADA WA VITI MWENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU
DIWANI KATA YA ZINGIZIWA ATOA MSAADA WA VITI MWENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU
Na Mwandishi Wetu DIWANI wa Kata Zingiziwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Salehe Kaniki ameendelea kugusa maisha ya makundi mbalimbali yenye uihitaji maalum. Miongoni mwa makundi ambayo Diwani Kaniki ameyagusa na kuyafikia ni kundi la watu wenye mahitaji maalum ambapo leo Mei 22,2026 amekabidhi vitimwendo (baiskeli) viwili na viti vya kusukuma vitano na magongo kwa watu wenye ulemavu. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Diwani Kaniki amesema amefanikisha kufikisha msaada huo kwa walengwa kupitia ushirikiano kati yake na wenyeviti wa Serikali za mtaa katika kata hiyo kwa kuorodhesha walengwa na leo wamekabidhi msaada huo. “Tumekutana kwa dhumuni moja la kusaidia ndugu zetu wenye uhitaji maalum ambao hawawezi kutembea ,tumekabidhi baiskeli mbili na viti vya kusukuma vitano kwa ujumla wake tumewafikia watu saba lakini tumetoa na magongo ya kutembelea. “Kwahiyo kuna magongo mengine tumeweka ya ziada lakini kuna wengine wamejitokeza na tumeandika…