DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN KILO 504.36 ZATEKETEZWA KATIKA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE
DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN KILO 504.36 ZATEKETEZWA KATIKA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE
-Ni dawa zilizokamatwa ndani ya jahazi la Al Arab lililokuwa na raia saba wa Iran Bahari ya Hind Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza kilogramu 504.36 za dawa za kulevya aina ya heroin katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara. Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa uteketezaji huo umefanyika kutokana na amri ya Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mtwara baada ya kukamilika kwa hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa waliohusika na dawa hizo. Dawa hizo zilikamatwa ndani ya jahazi la Al Arab lililokuwa na raia saba wa Iran katika Bahari ya Hindi ndani ya eneo la kiuchumi la Tanzania. Uteketezaji huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Sura ya 95 inayoruhusu kuteketezwa kwa vielelezo vya dawa za kulevya baada ya taratibu za kisheria kukamilika au wakati shauri linaendelea kwa idhini ya mahakama. Katika hatua nyingine Mamlaka imeendelea kusisitiza umuh…