CCM YAFUNGA KAMPENI ISIMANI KWA KISHINDO, YATANGAZA IMANI KUBWA KWA EMANUELA MTATIFIKOLO
CCM YAFUNGA KAMPENI ISIMANI KWA KISHINDO, YATANGAZA IMANI KUBWA KWA EMANUELA MTATIFIKOLO NA DENIS MLOWE , MIGOLI CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimehitimisha rasmi kampeni zake za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Isimani kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika eneo la Migoli, ambapo viongozi wa chama walionesha matumaini makubwa ya kupata ushindi kupitia mgombea wake wa ubunge, Emanuela Mtatifikolo. Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa kufunga kampeni, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Mary Chatanda, aliwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, akieleza kuwa chama kimefanya kazi kubwa ya kuwafikia wapiga kura katika maeneo yote ya jimbo hilo. Chatanda alisema ushindi wa CCM utatokana na ushirikiano wa wanachama na wananchi, huku akiwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha familia zao kushiriki uchaguzi huo. Mratibu wa kampeni za CCM katika uchaguzi huo, Solo Kasaba, alisema chama kimeendesha kampeni zake kwa mafanikio katika kata zote za jimbo hilo, kikifanya mikutano mi…