BHALONDO WAVUNJA REKODI YA UCHANGIAJI KYELA IBHASA FESTIVAL

BHALONDO WAVUNJA REKODI YA UCHANGIAJI KYELA IBHASA FESTIVAL
Na Mwandishi Wetu KUELEKEA msimu mwingine wa Tamasha la Kyela Ibhasa Festival linalofanyika kila mwisho wa mwaka wilayani Kyela mkoani Mbeya, kikundi cha wazawa wa Kyela kiitwacho Bhalondo kimeweka rekodi mpya ya uchangiaji baada ya kufanikisha kukusanya shilingi milioni 2.85 kwa ajili ya maandalizi ya tamasha hilo. Rekodi hiyo imekuwa ya kipekee tangu kuanzishwa kwa umoja huo, huku kikundi hicho chenye wanachama 19 kikionekana kuwa mfano wa kujitolea na mshikamano katika kuendeleza shughuli za kijamii na maendeleo ya nyumbani kwao. Kwa mujibu wa wanakikundi hao, mafanikio hayo yametokana na utaratibu waliouweka wa kuchanga fedha kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kuhakikisha kabla ya mwezi Juni tayari wanakuwa wamemaliza mchango wao, ili muda unaobaki uwe wa kujipanga zaidi kwa ajili ya kufanikisha tamasha hilo litakalofanyika mwezi Desemba mwaka huu. Mtunza Hazina wa kikundi hicho, Janeth Mophaty, amesema siri ya mafanikio yao ni moyo wa uzalendo na dhamira ya dhati ya kuipenda Kyela pam…