ALUMNI WA CBE WAHIMIZWA KUCHANGIA MAENDELEO YA TAIFA

ALUMNI WA CBE WAHIMIZWA KUCHANGIA MAENDELEO YA TAIFA
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM WAHITIMU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) (alumni) wametakiwa kutumia nafasi zao kuchangia maendeleo ya taifa kupitia taaluma, uzoefu na rasilimali walizonazo. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Kibaha Prof. Marcellina Chijoriga wakati akizungumza katika hafla ya Alumni Breakfast iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo alieleza kuwa alumni ni rasilimali muhimu ya kimkakati kwa maendeleo ya elimu na uchumi. Amesema mafanikio ya taifa hayawezi kutegemea juhudi za Serikali pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali wakiwemo alumni wenye mchango mkubwa katika jamii. “Alumni si wahitimu wa zamani tu, bali ni nguvu ya mabadiliko. Kila mmoja ana jukumu la kuendelea kutoa mchango wake katika kujenga taifa,” amesema Prof. Chijoriga. Amebainisha kuwa alumni wana nafasi kubwa ya kusaidia maendeleo ya wanafunzi na taasisi kupitia ushauri wa kitaaluma, kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa vitendo, ajira, pamoja na kushiriki katika …