WMA YAENDELEZA UKAGUZI WA VIPIMO KUDHIBITI UFUNGASHAJI USIOZINGATIA VIPIMO SAHIHI
WMA YAENDELEZA UKAGUZI WA VIPIMO KUDHIBITI UFUNGASHAJI USIOZINGATIA VIPIMO SAHIHI
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) wamekamata magari mawili yaliyokuwa yamepakia mazao kwa kutumia magunia yenye uzito unaozidi kipimo kinachoruhusiwa, katika operesheni ya kushtukiza iliyofanyika katika masoko ya Ilala na Temeke, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 4, 2026, Meneja wa WMA Mkoa wa Ilala, Muhono Nashon, amesema magari hayo yalibeba magunia yenye uzito wa kati ya kilo 170 hadi 200, kinyume na uzito rasmi usiozidi kilo 100 kwa kila gunia. Amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za vipimo na kinaathiri haki ya wafanyabiashara pamoja na watumiaji. “ Uzito unaotakiwa ni usiozidi kilo 100 kwa kila gunia, lakini tumekuta baadhi ya magunia yamezidi hadi kilo 200, jambo ambalo si sahihi,” amesema Nashon. Nashon ameeleza kuwa wafanyabiashara waliokutwa na makosa wamepewa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia vipimo sahihi, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo litaendelea kufanyika mara kwa mara ili kudhibiti ukiukwaji huo. Ameon…