WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATOA MAFUNZO USULUHISHI WA NDOA MKOANI KAGERA
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATOA MAFUNZO USULUHISHI WA NDOA MKOANI KAGERA
Na Diana Byera, Bukoba WIZARA ya Katiba na Sheria imeanza kutoa mafunzo kwa wajumbe wa bodi za usuluhishi wa migogoro ya ndoa, kutokana na ongezeko la kesi za talaka nchini, Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria Franklin Rwezimula amesema mafunzo hayo yameanzia mkoani Kagera kwa lengo la kuongeza weledi na mbinu mpya za usuluhishi wa ndoa katika jamii ili kujenga familia bora na jamii yenye mshikamano “Takwimu zinaonyesha talaka zilizosajiliwa mwaka 2023 zilikuwa 711, mwaka 2024 zikapanda hadi 1,569, na mwaka 2025 talaka zilizosajiliwa zilikuwa 1,172 na hizo ni zile talaka tu zilitoleawa taarifa na ndoa nyingine zimekuwa zikivunjika kimya kimya bila kutolewa taaarifa na kuhatarisha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.” Amefafanua bodi za usuluhishi zinapaswa kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha kuwa mahakimu huku akidai bodi hizo zisiwe sehemu ya kupokea rushwa Bali zijikite kuondomitafaruku kutovujisha Siri na Kutenda haki. Kwa upande …